Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:47 am

NEWS: WABUNGE WASTUKIA KUFIKIWA KWA MALENGO YA MILENIA

DODOMA: WABUNGEwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamesema utekelzeaji wa malengo endelevu ya Milenia hayawezi kutekelezwa kutokana na vipaumbele vilivyowekwa kutozingatia mahitaji ya taifa.

Wakizungumza leo mjini hapa katika semina ambayo iliandaliwa na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), baadhi ya wabunge wamesema kuwa malengo hayo hayakuangalia nini kilitakiwa kupangwa kwa wakati huo.

Mbunge wa Mbozi Paschal Haonga (Chadema) alisema malengo hayo yangeendana na ongezeko la uchumi wa kilimo lazima kungekuwa na mabadiliko lakini suala la kutaja kuongezeka kwa uchumi kwa kutumia makaratasi halina maana kw amalengo endelevu.

Haonga amesema kwa sasa kilimo kinashuka badala ya kupanda hivyo kuonyesha mashaka makubwa kuhusu utekelezaji wake kwani mkazo ungewekwa katika kilimo hali ya umasikini ingepungua kwa asilimia 50.

Naye Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulya (CUF), amesema malengo 17 yanayotangazwa na serikali yatapata ugumu wa utekelezaji wake badala yake yataishia kuwa kwenye vitabu.

Mtulya amesema malengo hayo yalichukuliwa kutoka nchi za kigeni badala ya kuweka mkakati wa kuyapanga malengo yao katika taifa.

Amesema Malengo katika matamko yanaonekana kuwa mazuri, lakini ukweli ni kuwa yamechukuliwa kutoka kwa wenzetu badala ya kuangalia vipaumbele vyetu jambo ambalo litakuwa gumu.

Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwanko (CCM) amesema malengo endelevu yapo kwa ajili ya kuyainua baadhi ya mataifa lakini kwa Tanzania itakuwa ni ngumu kufikia malengo yote.

‘’ Taifa linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa ili kulifanya lisonge mbele lakini kwa namna malengo hayo yalivyowekwa huenda ikawa ni vigumu kuyafikia’’alisema

Akijibu baadhi ya hoja mmoja ya Wawezeshaji katika semina hiyo Ambrose Mugisha amesema mipango iliyowekwa katika malengo hayo ni mizuri na inapaswa kusimamishwa kikamilifu lakini akasema wabunge wanayo fursa nzuri ya kufanya mapinduzi katika mafanikio.

Mugisha amesema kwa sasa dunia inakwenda katika sayansi na teknolojia ambapo imekuwa kiganja hivyo akaomba wabunge kutumia nafasi zao kikamilifu katika kuishauri na kuisimamia serikali.