- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WAOMBA MIONGOZO YA KUSITISHA SHUGHULI ZA BUNGE
Dodoma: KUTOKANA na matukio mbalimbali ambayo yanatokea hapa nchini wabunge wengi wamelazimika jana bungeni kusimama na kuomba miongozo kwa spika kwa lengo la kuhairisha shughuli za bunge.
Hali hiyo ilijitokeza muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni.
Wabunge walioomba miongozo ni pamoja na mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani, maarufu kwa jina la Prof Maji marefu,James Mbatia (NCCR Mageuzi) na Rashid Shangazi (Mlalo-CCM).
Akizungumza Ngonyani maarufu kama Majimarefu alitumia kanuni ya 68(7) alisema kuwa kuna matatizo makubwa ya mafuriko nchini.
“Haswa kwenye mkoa wangu wa Tanga, kumekuwa na maafa, leo hii tunavyoongea kuna watu 1000 hawana chakula, mahali pakuishi na hawana msaada wowote lakini itawasaidiaje hawa watu wakati kamati za afya zikiendelea na utaratibu,”alisema.
Alisema watu wanaadhirika na wanaweza kufa wakati wote.
Naye Shangazi alisema anasimama kwa kanuni 47 (1) akitaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili kuhuau mafuriko hayo.
“Sasa hivi katika mkoa wa Tanga kuna mafuriko makubwa sana. Na jana
yametokea maporomoko katika milima ya usambara, eneo la barabara Lushoto- Arusha- Mombo , Pangani kwenda Tanga, Mombo kwenda Lushoto na Kilindi kwenda Morogoro shoto zilifungwa,”alisema Shangazi.
Alisema Mkoa wa Tanga umegeuka kuwa kisiwa umepata athari kubwa hasa Korogwe na kuiomba Serikali ilione hilo jambo ni la kimkakati na kwamba Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroad) amezidiwa .
Alisema barabara hizo zimekuwa zikiunganisha mkoa huo na mikoa mingine na kutaka Bunge lijadili angalau kwa muda mchache.
Kwa upande wake , Mbatia alisema hali ni tete ikiwemo Kilimanjaro, mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Zanzibar kufuatia mafuriko yaliyojitokeza na kuomba utu wa mwanadamu kuzingatiwa kama wawakilishi wa Watanzania kwa kutenga muda wa angalao dakika 15 kujadili suala hilo.
“Tutenge muda wa dakika 15 ama 20 ili tujadili suala hili a,mbayo ni ya
maafa tunaweza tukatoa majibu ni sahihi kwa wapiga kura wetu, mheshimiwa mwenyekiti ndio ombi langu kwa mujibu wa kanuni nilizozitumia,”alisema.
Akijibu miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, alisema kuwa miongozo ya Mbatia na Shangazi imeangukia katika kanuni ya 47(1) ambayo inasomwa pamoja na kanuni ya 48.
“Lakini kanuni ya 47(4) inampa Spika mamlaka aridhike kama ombi hilo anaona jambo hilo kweli linahitaji kusitisha shughuli zilizombele yetu ili
kujadili hoja hizo za dharura,”alisema.
Hata hivyo, alisema kwa hali anayoiona haoni kama suala hilo kama suala
hilo linahitaji kujadiliwa sasa.
“Ni kweli tukio hili limegusa maeneo mengi nawapa pole walioguswa kwa namna moja hata nyingine.. Naamini Serikali iliyoko humu ndani itaitolea maelezo wakiangalia nchi nzima,”alisema.
Alisema anaamini Serikali italizungumzia vizuri kuliko kila mbunge
kujisemea katika eneo lake.
Kwa upande wa Ngonyani, Chenge alisema kwa mujibu wa kanuni ya 68(7) ni lazima liwe tukio ama jambo ambalo limetokea mapema bungeni na si nje.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge
wakati akiji bu Mwongozo wa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo) Zitto Kabwe.
Akiomba mwongozo bungeni, Zitto alisema michango ya wabunge kwa sioku tatu inataka bajeti ya Wizara ya Maji na Mifugo kwa mwaka wa fedha 2017/18 iongezwe na wametoa mwongozo iongezeke kwa kiasi gani na fedha zitoke wapi.
“Kitabu cha maendeleo cha nne utaona sehemu kubwa ya kupungua kwa bajeti ya wizara ya maji ni kwenye eneo la Rural Water Supply and Sanitation (Usambazaji wa maji vijijini na majitaka), utaona kwamba bajeti ya ndani la miradi ya maji limepungua kwa Sh 282 bilioni katika hizo Sh 152 bilioni ni maji vijijini pekee na Sh 88 bilioni ni kwa ajili ya jiji la Dar es Salaam pekee,”alisema.
Alisema wabunge walikuwa wanataka kuongeza Sh 50 ambayo itaweza kufidia pengo linalotokana na bajeti hilo.
Alisema wakipitisha bajeti hiyo bila kuleta marekebisho yatakayoingiza
fedha hizo itakuwa hakuna maana na kwamba Waziri wa Fedha na Mipango atakapokuja anaonyesha hizo fedha katika kitabu cha mapato.
Alihoji kama mwenyekiti haoni kuwa kabla ya kuendelea na mjadala wa bajeti hiyo wapate marekebisho yatakayoelekeza hizo fedha zinazopatikana (zilizopungua) ili wabunge watakapopitisha bajeti hiyo waweze kuwa fedha iliyoongezwa.
Akijibu Chenge alisema kuwa ni kweli kwa muda wa siku mbili wabunge
wamekuwa wakichangia bungeni wametoa ushauri wa kuongeza bajeti ya maji kwa Serikali.
“Lakini kwa pointi inayopendekezwa na Zitto mimi sitakubali tufike huko,
kwanini nasema hivyo? Kanuni zetu za Bunge kupitia Kanuni ya 105, mnaona taratibu uliowekwa ni mzuri sana,”alisema
“Kamati ya Bajeti na Serikali ina siku saba za kushauriana tena kwa kina na si kwa hoja hii tu. Kuna hoja hizo ambazo tulianza nazo. Kupitisha fungu leo, jana hakumanishi kwamba fungu hilo haiwezi kufunguliwa.”
Alisema kitakachofanyika baada ya kamati ya bajeti na Serikali kukubaliana ni maeneo gani ambayo wanaweza kuongeza fedha, Serikali itakuja na marekebisho ya mafungu ya bajeti siku itakayoleta bungeni appropriation bill ingawa hautajadiliwa.
Alisema muswada huo utakuja na maeneo ambayo yameongezewa fedha na kwamba mwongozo wake ni wasiende kwa kupitia kanuni ya 69(1) na
badala yake watumie Kanuni 105 ili kuipa muda kamati ya bajeti na
Serikali kutendea haki wizara hiyo na sekta nyingine.