- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WALILIA BIMA YA AFYA YA MAISHA
Dodoma: Wabunge wameshangazwa kitendo cha ofisi ya bunge kupitia Jumuiya ya Madola(CPA) kushindwa kuwapatia bima ya maisha wabunge ambao wanamaliza muda wao kama umoha huo unavyotaka.
Mbunge wa Mwibala,Kangi Lugola (CCM) ndiye aliyekuwa wakwanza kuibua mjadala huo leo bungeni wakati walipokuwa wakichangia muda mfupi baada ya wawasilisha mada kutoka CPA.
Naye mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) amesema wabunge wamegeuzwa kuwa sawa na ATM kwa kuwa imesengeka dhana kila mbunge anayo hela nyingi zaidi ya kusaidia jamii.
Mbali na hilo amesema wabunge wanashindwa kutimiza wajibu wao kutoka na wabunge kijifafanya sehemu ya serikali badala ya kutambua kuwa wao wajibu wao ni kuisimamia serikali katika kufanya shuguli za maendeleo.
Naye Mbunge wa Same Mashariki,Nagenjwa Kaboyoka (Chadema)amesema anashangazwa kuona Tanzania ndiyo makao makuu ya Jumuiya ya Madola na Spika wa Tanzania ndiye rais.
Naye mbunge wa Songwe, Philipo Mlugo (CCM),amesema katika maelezo ya watoa mada walieleza katika Jumiya hiyo kuwa Waziri Mkuu ni Mlezi na Spika wa Bunge ni rais wa Jumuiya.
Kutokana na maelezo hayo Mulugo alitaka kujua nini majukumu ya Waziri Mkuu na Nini majukumu ya Spika kwani Jumiya ya Madola kwa Bunge la Tanzania ni kama limekufa.
Pia amewataka iwekwe bayana utofauti wa viwango vya malipo kati ya nchi ya Kenya na Tanzania kwani kunaonekana Bunge la Tanzania halitimizi majukumu yake ipasavyo licha ya kuwa wabunge wanakatwa kodi nyingi katika mishahara pamoja na magari.
Hata hivyo Mulugo amehoji ni kwanini wabunge wanakatwa kiasi cha sh.milioni moja laki mbili kama kiinua mgogo cha mbunge na ni nani aliyetoa kibali hicho.
Akijibu hoja hizo Said Yakubu, amesema ni haki ya mbunge apata bima ya afya ya maisha kwani sheria zinaelekeza hivyo.
Aidha amesema kitendo cha wabunge wa Tanzania kugeuzwa kama ATM ni mapenzi yao wenyewe kwani wabunge badala ya kuibana serikali na kushinikiza serikali ipeleke maendeleo wamekuwa wakifanya wenywe wabunge.
Katika semina hiyo ya wabunge ambayo lengo kuu lilikuwa kuwapatia elimu na maelekezo juu ya umuhimu wa mabunge ya jumuhiya ya madola kazi zake na kuona kama utendaji wa mabunge hayo unaendana na utendaji wa Bunge la Tanzania.
Waliotoa semina hiyo ni Said Yakubu na Prof,David Mwamfupe.
Katika semina hiyo Yakubu alitoa mada juu ya Muundo,Shughuli na Majukumu ya Jumuiya ya Madola.
Amesema jumuiya ya madola ni umoja wa hiari wan chi 52 ambazo zilipata kuwa koloni la mwingereza isipokuwa nchi ya Rwanda na Msumbiji ambazo ziliomba kwa hiari kujiunga.
Amesema nchi hizo za jumuiya zinajumuisha nchi ambazo zina ucumi mkubwa,visiwa vidogo 30 vyenye idadi ya watu wasiozidi 100,000.
Kuwa kitengo cha utafiti ya masuala ya Anuai yahusuyo bunge ulibaini masilahi mabalimbali ambayo utolewa kwa wabunge katika nchi mbalimbali.
Amesema katika nchi ya Kenya mbunge analipwa mshahara sawa na wa katibu mkuu wa Wizara, wanalipwa posho ya nyumba, mahudhurio, takrima ya nyumba na gharama za Jimbo.
Naye Prof Mwamfupe amesema malengo ya CPA katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu(SDGs).
Amesema ni malengo ya matamanio ya ulimwengu yanayokusudiwa kupeleka maendeleo ya Kiuchumi,ujumuishwaji wa kijamii na endelevu wa mazingira.