- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WAISHUKIA SERIKALI KWA MADAI YA KUZIBAGUA SHULE ZA BINAFSI
DODOMA: Wabunge wameishukia serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia na Ufundi kwa madai kuwa imekuwa na tabia ya kuzibagua shule za binafsi.
Mmoja wa wabunge waliochangia katika hotuba ya Wizara hiyo mbunge wa Songwe, Philipo Mlugo (CCM)alisema ni kwanini serikali imekuwa ikizibagua shule za za watu binafsi.
Akizungumzia suala kodi za shule alisema serikali imekuwa ikitoza kodi nyingi katika shule za binafsi licha ya kuwa shule hizo nazo zinatoa mchango mkubwa kwa serikali.
Akizungumzia suala la usambazaji wa vitabu vyenye makosa alisema jambo hilo ni aibu kwa serikali kwani kosa hilo linaonesha wazi kuwa umakini kupitia kwa wataalamu ulikuwa mdogo.
Mlugo alisema anashangazwa na tabia ya wakaguzi wa serikali kwa kuonesha uonevu wa wazi wazi kwa shule za binafsi.
Alisema sera inaonesha kuwa darasa moja linatakiwa kuwa na wastani wa wanafunzi wapatao 45, lakini
Naye mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema)alisema licha ya kuwa hakuna mtu ambaye anakubaliana na kuwepo kwa vyeti vya kugushi lakini anaye pewa lawama kubwa ni Baraza la Mitihani.
Waitara alisema serikali imekuwa ikibadilisha sana mitahara ya kufundishia jambo ambalo linawafanya walimu kushindwa kufanya makazi yao.
Hata hivyo Mwita alisema kwa sasa serikali inadaiwa fedha nyingi na walimu jambo ambalo linasababisha walimu kukatatamaa ya kuwafundisha.
Kwa upande wake mbunge wa Urambo,Magreth Sitta (CCM)alipendekeza serikali ione uwezekano wa watoto wa kike ambao wamebeba mimba warudishwe mashuleni.
Mbali na hilo mbunge huyo aliishauri serikali kuhakikisha kila shule ambayo inatakiwa kusajiliwa iwe miundombinu ya maji ili kuondokana na tabia ya watoto kubebelea vidumu vya maji.
Alisema kitendo cha kutowapeleka shule kutokana na kubeba mimba ni kuwanyima haki yao ya kupata elimu huku watoto wanaotokana katika familia masikini.
Akichangia bungeni mbunge wa Viti Maalum, Ruth Mollel (Chadema)ameitaka serikali kuona uwezekano wa kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia ili kuondoa mkanganyiko wa kutokuwa na uelewa lugha gani ambayo inafaa kufundishia.
Akizungumzia mfumo wa elimu nchini alisema bado mfumo huo haujakaa sawa katika kumfanya mtoto wa kitanzania kupata elimu ambayo inaonekana kuwa na manufaa zaidi.
Akichangia mbunge wa Ulanga Mashariki,Godruck Mlingwa (CCM) alisema kutokana kilio kikubwa cha walimu kuidai serikali yeye atakuwa balozi wa walimu na kamwe hatatoka bungeni hadi matatizo ya walimu yatatuliwe.