Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:49 am

NEWS: WABUNGE WAFUNDWA.

DODOMA: WABUNGE wametakiwa kusimamia serikali kwa hoja ili kukamilisha malengo endelevu(SDGs).

Kauli hiyo ilitolewa jana na ofisa wa bunge Dikson Bisile alipokuwa akitoa semina kwa wabunge wa kamati mbalimbali juu ya utekelezaji wa malengo endelevu.

Akitoa semina hiyo iliyofadhiliwa na UNDP,Bisile alisema kazi kubwa ya wabunge ni kuisimamia serikali pamoja na kusimamia malengo endelevu 2030.

Akitoa masemina hiyo alisema katika kutekeleza malengo endelevu ni vyema wabunge wakasimamia kwa njia sahihi masuala ya utawala bora,demokrasia,maendeleo ya mikopo pamoja na maendeleo ya sehemu husika

Hata wabunge wamesema siyo rahisi wabunge kutekeleza malengo endelevu kwani serikali haikubali kushauriwa badala yake inakandamiza bunge.

Mbunge wa ukonga Mwita Waitara (Chadema)alisema wabunge wengi ni waoga wa kuishauri na kuisimamia na nguvu zao zinaishia katika kamati au makubaliano katika semina.

Waitara akichangia katika semina hiyo alisema yako matatizo mengi lakini serikali haitaki kukosorewa.Naye mbunge wa Mwibala Kanggi Lugola CCM, alisema uharibifu wa miundombinu unachangia kutofikia malengo ya endelevu ya mileniam.Akichangia Salome Makamba Chadema,alisema yapo matatizo makubwa yanayochangia ikiwa ni pamoja na kuminya demokrasia.

Makamba aliogeza kuwa si jambo rahi kuwepo kwa malengo endelevu kwani demokraria imeminywa kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa ambayo inatoa fursa ya kukutana na jamii ili kujua changamoto zao.