Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:44 am

NEWS: WABUNGE WA VITI MAALUM WALILIA FEDHA YA MFUKO WA JIMBO.

Dodoma: WABUNGE wa Viti Maalum wameonesha masikitiko yao ya kukosa mgao katika mfuko wa jimbo licha ya kuwa nao wanafanya kazi kubwa ya kuhudumia wananchi.

Hali hiyo imejitokeza bungeni baada ya wabunge wa viti maalum walipokuwa wakiuliza maswali ya nyongeza na kuhoji ni kwanini serikali haitengi fedha kwa ajili ya kuwawezesha wabunge wanawake kama ilivyo wabunge wa jimbo.

Cecilia Paresso (Chadema) ni mmoja wa wabunge wa viti maalum,ambaye amehoji ni kwanini wabunge wa viti maalum hawapatiwi fedha kama ilivyo wabunge wa jimbo na wakati huo hawaruhusiwi kushiriki katika kamati za fedha katika halmashauri yao.

“Serikali imekuwa haitengi fedha kwa ajili ya wabunge wa jimbo licha ya kuwa wabunge wa viti maalum wana kazi kubwa sawa na wabunga wa jimbo lakini inaonesha wazi wabunge wa majimbo wanaogopa kutoa fedha katika mfuko wa jimbo kuwapatia wabunge wa viti maalum.

“Hali hiyo ya hofu inatokana na ukweli kuwa wabunge wa viti maalum wakipatiwa fedha wanaweza kuwang’oa wabunge wa majimbo”amesema Paresso

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum,Faida Mohamed Bakari (CUF) alitaka kujua ni lini serikali itarekebisha sheria ya mfuko wa jimbo ili kuweza kuwajumuisha wabunge wote ikiwemo wabunge wa viti maalum.

Akijibu maswali la nyongeza lililoulizwa na Paresso Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais –TAMISEMI, George Simbachawene amesema kuwa mfuko wa jimbo uko kisheria na unawahusu wabunge wa jimbo.