- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WA TANZANIA KUINGIA KWA MAFUNGU MBUNGENI
Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema Mkutano wa Bunge unatarajiwa kuanza kesho Jumanne Machi 31, 2020 mjini Dodoma lakini kutakuwa na utaratibu tofauti wa uendeshaji wa chombo hicho, lengo likiwa ni kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Machi 30, 2020 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema vikao vya mkutano huo wa 19 Bunge la 11 vitaanza kesho na kumalizika Juni 30, 2020 lakini kutakuwa na mabadiliko makubwa ikiwemo la kikao kuanza saa 8 mchana na kumalizika saa 12 jioni, badala ya kuanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 1:30 jioni.
Amesema katika mikutano mingine walikuwa wakikutana kwa saa 9 ama zaidi lakini katika mkutano huo watakutana kwa saa zisizozidi nne.
Amesema nyaraka zote kutoka serikalini zitawafikia wabunge na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao.
Amesema kesho kikao kitaanza saa 3 asubuhi kwa sababu Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akiahirisha mkutano wa 18 wa Bunge alisema kuwa anaahirisha hadi saa 3:00 asubuhi.
“Kuanzia keshokutwa tutaanza saa 8 mchana..., kwa hiyo ndani ya Bunge kutakuwa na wabunge wasiozidi 150 kwa wakati kutoka ile namba niliyosema ya zaidi ya watu 700,” amesema.
Amesema mawaziri wote watazungumza kutoka alipokaa kwa kutumia kipaza sauti na si kwenda mbele kwenye mimbari kama ilivyozoeleka.
“Hakutakuwa na maswali na majibu kama ilivyozoeleka. Yote yataingizwa katika mtandao wa tablet za wabunge asubuhi ya siku husika. Na kama mbunge ana maswali ya nyongeza ataandika na swali litaingia katika mfumo wetu wa Bunge,” amesema.
Amesema mawaziri watapata maswali hayo na kabla ya saa 7:00 mchana yatakuwa yamewafikia wabunge.
Amesema hakutakuwa na maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu katika mkutano wote wa Bunge.
Amesema wabunge wengine ambao hawataingia katika ukumbi wa Bunge, wataingia katika kumbi nyingine zilizoandaliwa na watafuatilia vikao vya Bunge kwa njia ya video.
Ndugai amesema wataweka utaratibu ambao kila mbunge ataweza kupiga kura bajeti ya mwaka 2020/21 kupitia tablet yake.
Amesema siku ya kupitisha bajeti kuu kikatiba kila mbunge anatakiwa kupiga kura, hivyo wataweka utaratibu ambao wabunge wataingia kwa awamu kwa ajili ya kupiga kura.