- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WA MAREKANI WANAMCHUNGUZA TRUMP KUIUZIA SAUDIA NUKLIA
Wabunge nchini Marekani wamesema wanaanza uchuguzi wa kumchunguza Rais Donald Trump kama anajaribu kuuza teknolojia nyeti ya nyuklia ya nchi hiyo kwa taifa la Saudi Arabia,kwa lengo la kuwafurahisha wafanyabiashara na wafuasi wake ambao wanaomuunga mmkono.
Bunge la Marekani tayari limeshafungua uchunguzi dhidi ya pendekezo la utawala wa Trump, la kutaka kujenga vituo kadhaa vya kinyuklia nchini Saudi Arabia.
Mwakilishi Elijah Cummings, mwenyekiti wa Kamati ya Halmashauri ya Uangalizi na Mageuzi, ameitaka Ikulu ya Marekani kuwasilisha nyaraka ikiwa zile zinazohusu mkutano uliofanyika miezi miwili tu baada ya Trump kuingia madarakani kati ya mkwewe, Jared Kushner, na mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia , ambae muda mchache baada ya mkutano huo alitangazwa mrithi wa ufalme wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Ripoti ya Kamati ya Uangalizi ya Baraza la Wawakilishi imesema mshauri wa zamani wa usalama wa taifa Michael Flynn na wenzake wawili walipendekeza mpango huo kwa Tom Barrack, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya kuapishwa kwa rais, na muungano wa makampuni ya Marekani yakiongozwa na makamanda wa kijeshi waliostaafu na viongozi wa zamani wa Ikulu ya Marekani.
Juhudi za mpango huo, ripoti imesema zilianza kabla ya Trump kuingia madarakani na kuendelea hadi baada ya kuapishwa kwake Januari 2017, licha ya wafanyakazi wa Baraza la Usalama wa Taifa kuonya kwamba uhamisho wa teknolojia ya nyuklea ya Marekani kwenda Saudi Arabia unaweza kuangaliwa kama uvunjaji wa Sheria ya Nishati ya Atomiki.