Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:36 pm

NEWS: WABUNGE WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WASUSIA KUAPISHWA KWA MBUNGE WA VITI MAALUM CUF

Dodoma: Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani wamesusia kushuhudia kuapishwa mbunge wa viti maalum CUF Rehema Juma Migila huku spika wa Bunge Job Ndugai akiagiza kukamatwa na kuitwa kuhojiwa na kamati ya maadili na madaraka ya bunge kwa baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Ubungo Said Kubenea na mbunge wa Kigoma Mjini Zito Kabwe kwa tuhuma mbalimbali.

Ni katika bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linaloendelea na vikao vyake hapa mjini Dodoma ambapo kabla ya taarifa ya spika kutolewa wabunge waliweza kushiriki katika kipindi cha maswali na majibu ambapo kabla ya kipindi hicho wabunge wa upinzani hawakuingia ndani ya bunge kushuhudia zoezi la kuapishwa kwa mbunge huyo

Akizungumza nje ya ukumbi wa Bungekwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni, mbunge wa vitimaalum Suzan Lyimo amesema wataendelea na msimamo huo kwani bado kuna mgogoro unaoendelea huku mbunge aliyeapishwa Rehema Juma Migila akidai kuwa yeye ni mteule halali huku akiomba wenzake kutoa ushirikiano na kuacha uadui

Aidha katika hatua nyingine spika ameagiza kuitwa na kuhojiwa mbunge wa jimbo la ubungo Saed Kubenea ili athibitishe taarifa ambazo amezisema kuhusu kushambuliwa kwa risasi mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu kwa risasi.

Aidha, Spika ndugai amemtaka mbunge wa kigoma mjini Zito Kabwe, kuripoti katika kamati ya maadili na madaraka ya Bunge kutokana na tuhuma za kuashifu Bunge

Pia bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2017.

Bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania bado linaendelea na vikao vyake hapa Dodoma kwa ajili ya kupokea miswada mbalimbali ya sheria na linataraji kuahirishwa mapema Sept 15 Mwaka huu