Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:46 pm

NEWS: WABUNGE WA CHAMA CHA THERESA MAY WAMTAKA KUJIUZULU

Waziri mkuu wa uingereza Bi .Theresa may anakabiliwa na shinikizo kali kutoka kwa wabunge wa chama chake wakimtaka kujiuzulu baada ya moja kati ya Mawaziri wake wa juu kujiuzulu.

Kiongozi wa baraza la wawakilishi nchini Uingereza Andrea Leadsom amejiuzulu.

Image result for theresa may

Leadsom amesema hana imani tena na njia anayotumia Waziri Mkuu Theresa May kama inaweza kuufanikisha mchakato wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya ama Brexit. Hatua hiyo inaongeza shinikizo kwa waziri mkuu May. Leadsom, anayetambulika zaidi kwa kuunga mkono Brexit amemuandikia barua waziri mkuu May akimtolea mwito wa kuchukua maamuzi sahihi kwa ajili ya maslahi ya taifa, serikali na chama chao.

Kujiuzulu kwake kunakuja siku moja kabla ya Uingereza kushiriki uchaguzi wa bunge la Ulaya.

Image result for theresa may

May amewaambia wabunge kuwa wana nafasi ya kipekee ya kuwapa wananchi wa taifa hilo uamuzi wa kujiondoa kwenye Umoja huo au la wanaweza kuamua, kufanyike kwa kura ya pili ya maoni.

Mawaziri wengine kadhaa wamenukuliwa wakisema kuwa Waziri Mkuu hawezi tena kubaki katika wadhifa huo, kauli ambayo imeungwa mkono na Jeremy Corbyn kiongozi wa upinzani kupitia chama cha Labour.

Uingereza imepewa na Umoja wa Ulaya had mwisho wa mwezi Oktoba kukubaliana kuhusu mkataba uliofikiwa kati ya nchi hiyo na vongozi wa Umoja wa Ulaya.

Wabunge kwa nyakati tatu tofauti, wamekataa mkataba wa Waziri Mkuu May wakimtaka afanye mazungumzo zaidi na wakuu wa EU.