Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:46 pm

NEWS: WABUNGE WA CHADEMA WAMJIA JUU UMMY BAADA YA KUSEMA SEREKALI IKOTAYARI KUMTIBU TUNDU LISSU

Dar es salaam: Baada ya kauli ya Serekali jana kupitia Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Ummy Mwalim kusema kuwa Serekali iko tayari na haijashindwa kugharamia matibabu kokote pale Duniani mara baada ya kupata maombi kutoka kwa familia na madaktari wa hapa nchini kama wataona inafaa zaidi, kauli hiyo imepigwa vikali na viongozi kadhaa wa upinzani,na hawa ni baadhi yao

Mbunge wa Tarime Mjini John Heche

Heche amehoji kwa serekali kuwa hakuna utaratibu wa mbunge yoyote kwenda kufanya maombi ya kutaka kutibiwa "Tangu lini familia ya mbunge inatuma Maombi Serekalini kwenda kutibu Mbunge ameumwa ? watanzania tuendelee kumchangia. aliandika Heche kwenye Ukurasa wake wa twitter

Henche amesema kuwa hii ni Wiki ya pili tangia Lissu ashambuliwe na kuumizwa vibaya ndio serikali inajitokeza kusema iko tayari kumtibu!! "inaudhi na kukera katika hili naona serikali inaona aibu baada ya wananchi kujitokeza na kusimama imara kuokoa maisha ya Lissu,wananchi kuanzia wenye kipato cha chini wamechanga kumtibu Lissu,


Heche anaona kuwa Tamko hili la serikali litakua na malengo ya kukatisha Watanzania tamaa kuendelea kuchangia matibabu ya Lissu, "tusikubali Watanzania tuendelee kuchangia ili mhe Lissu na Dunia ijue kwamba ninyi wananchi ndio mliomtibu Lissu na kwamba mnapinga unyama aliofanyiwa kamanda wetu ambae maisha yake yote ameyatoa kupigania wanyonge. ...kwasasa serikali ituambie nani waliomshambulia na kumuumiza Lissu vibaya
...wako wapi na wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa!" alisema Heche

Mchungaji pita msigwa

Kwa upande wake mbunge wa Iringa Mjini baada ya kauli ya Waziri Ummy yeye amesema kuwa anaona kama serekali ya awamu ya Tano inafanya utani kwenye swala la Tindulisu "HUU NI UTANI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO!"

Godbless Lema

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa upande wake ameanza kwa kuhoji kuwa ni yupi wa kuandika barua ni mke wa Mbunge au nani anayetakiwa kuandika barua kudhibitisha kuwa huyu ni mbunge na anahitaji matibabu?, hakuna utaratibu kama huo katika kanuni za kibunge wa kuandika barua kama ikitokea mbunge yoyote akiumwa, "wakati bunge linakatibu wa bunge, bunge linaspika wa bunge ambaye ni mkuu wa wabunge waote, spika wa bunge alikuwepo wakati lissu akisafirishwa kutoka Dodoma kuja Nairobi, anajua lissu alikoelekea, lakini mpaka leo hajawahi kuja Nairobi" alisema Lema kupitia vyombo vya habari.

Lema alimuonya waziri Ummy Kuwa asikubali kuagizwa, kwani yeye anafahamu kinachoendelea " Ummy usikubali kutumwa vitu kama hivi,unafahamu nini kinaendelea, na ndiomana serekali yenyewe pamoja na viongozi hakuna aliyepata ujasiri wa kuja kumsalimia mbunge ambae yupo taabani, kwa sababu wanajua jambo hili limetendwa na na kinanani, vinginevyo bunge lingekuwa la kwanza kulilia uhai wa Lissu'' aliongea Lema