- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WA CHADEMA WAGOMA KWENDA BUNGENI NA KUJIWEKA KARANTINI
Chama cha Upinzani cha Chadema nchini Tanzania kimewapiga marufuku wabunge wake wote kutoshiriki tena shughuli zozote za bunge zinazoendelea jijini Dodoma na Dar es salaam kwa hofu ya ugonjwa wa Corona(Covid-19).
Uwamuzi huo umetangazwa hii leo Mei mosi, 2020 na mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
"Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia Bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma, niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa." amesema Mbunge Ester Bulaya
Aidha chama hicho kimewataka wabunge wake wote walioko Dodoma kusalia huko na kujiweka karantini kwa siku 14 ili kuweza kubaina kama watakuwa na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona au la.
Waziri Mkuu wa Tanzania. Kassim Majaliwa juzi Aprili 29 alitangaza ongezeko la wagonjwa wa Corona 196 nchini, huku Tanzania Bara ikiwa na Wagonjwa 174 na Zanzibar wagonjwa 22 ambao walitolewa taarifa na Waziri wa Afya Wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na kufanya idadi ya wagonjwa wa Corona nchini kufikia 480.
Majaliwa alisema jumla ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 197, huku Zanzibar waliopona wakiwa 36 na Tanzania bara 83.
Pia Waziri Mkuu alisema kumekuwa na ongezeko la vifo vya watu sita (6) na kufanya kuwa na vifo vilivyotoka na Corona nchini kufikia 16. Kati ya wenye maambukizi 297 waliobaki, 283 wanaendelea vizuri na tiba na kusubiri ufuatiliaji wa afya zao na wengine 14 wako chini ya uangalizi maalumu wa madaktari ambao wanahitaji oksjeni (Oxygen) ya kuwasaidia kupumua pamoja na wale wenye magonjwa mengine ambayo yamejitokeza kwenye wodi.
Amesema Serikali imeendelea kuwaondoa washukiwa waliokua karantini ambao walishatimiza siku 14 baada ya uchunguzi wa kiafya kuonekana hawana maambukizi na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Hadi kufikia tarehe 28 Aprili, watu 644 wameruhusiwa kutoka karantini katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Zanzibar, Kilimanjaro, Mwanza, kagera, Songwe, Kigoma na Dodoma.