Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:43 pm

NEWS: WABUNGE NCHINI UINGEREZA WAGOMEA UCHAGUZI WA MAPEMA

Wabunge wengi nchini Uingereza wamekataa katakata pendekezo la waziri mkuu wa nchini hiyo Boris Johnson la kuitisha uchaguzi wa mapema mnamo Oktoba 15.

Tokeo la picha la england MP react agaist election

Katika kura iliyopigwa jana usiku, wabunge hao walikataa pia hoja ya Johnson ya kuiruhusu Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano mwezi ujao.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn, katika siku za nyuma alitaka uchaguzi mpya ufanyike, lakini chama chake kilijizuia katika kura ya jana.

Corbyn Amesema ataunga mkono uchaguzi mpya endapo tu uwezekano wa kuondoka bila ya makubalino utaondolewa. Wabunge wa upinzani wakiungwa mkono na wabunge waasi wa Conservative wanaonya kwamba Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano, kunaweza kusababisha madhara ya kiuchumi yasiyozuilika.

Johnson alisistiza siku ya Jumatano kwamba mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu makubaliano mapya, yamepiga hatua lakini muungano huo unasema hakuna mapendekezo mapya yaliyowasilishwa.