- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE AUTRIA WAMPIGA CHINI WAZIRI MKUU WAO
Wabunge nchini Austria leo Jumatatu Mei 27, 2019 wamefanya uwamuzi wa kihistoria baada ya kuiondoa madarakani serikali ya Kansela Sebastian Kurz baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Kura hiyo dhidi ya kiongozi wa nchi na serikali au baraza lake la mawaziri ni ya kihistoria nchini Austria tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Kura hiyo imeungwa mkono na wabunge kutoka chama cha Social Democrats na chama cha Freedom kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, ambacho kilikuwa katika serikali ya muungano ya Kurz hadi wiki moja iliyopita ambapo kiongozi wake alijiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa.
Kwa mujibu wa katiba, Rais wa Austria, Alexander Van der Bellen sasa anapaswa kumteua kansela mpya ambaye ataunda serikali ambayo itaungwa na mkono na bunge hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Kwamujibu wa katiba ya Austria Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.