- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE 5 WA CCM WALIMWA BARUA NA KATIBU WA CHAMA CHAO
Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amewalima Barua wabunge watano wa chama hicho Mkoani Shinyanga akiwataka kuandika barua ya kujieleza ''ni kwanini wasishukuliwe hatua za kinidhamu'' mara baada ya Kukaidi kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho kilichokuwa kikipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 Mkoani humo.
Wabunge waliolimwa barua ni pamoja na Ahmed Salum (Solwa), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Jumanne Kishimba (Kahama Mjini), Selemani Nchambi (Kishapu) na Lucy Maenga wa Viti maalum.
Kikao hicho kilifanyika juzi kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo pamoja na wajumbe wengine kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo, Zainab Telack.
Wabunge waliohudhuria na majimbo yao kwenye mabano ni Elias Kwandikwa (Ushetu) Ezekiel Maige (Msalala) na Azza Hilal Mbunge wa Viti Maalum.
Pia kikao hicho kilihudhuriwa ni mwenyekiti mmoja tu wa halmashauri ambaye ni Ngassa Mboje wa Wilaya ya Shinyanga.
Kutokana na hali hiyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa, alionyesha kukasirishwa na jambo hilo akisema kikao kilipaswa kuhudhuriwa na wajumbe 52 wa halmashauri kuu lakini ni 30 pekee waliojitokeza.
Magesa aliagiza wabunge na wenyeviti wa halmashauri ambao hawakuhudhuria waandike barua kwenda kwa makatibu wa wilaya na zimfikie.
“Naomba kila mwenyekiti wa halmashauri aniandikie barua kwanini hajafika kwasababu hapa anaonekana Ngassa Mboje Mwenyekiti wa Wilaya ya Shinyanga peke yake, wengine wako wapi? Sisi ndiyo tunateua madiwani kwahiyo msiwapende sana madiwani wakawakwamisha.
“Kwa kutumia nafasi niliyonayo tena kama Mkurugenzi wa uchaguzi wa mkoa huu, naomba wabunge ambao hawajahudhuria waandike barua za maandishi wajieleze kwanini hawapo, wasipojieleza tutaweka kumbukumbu na ikifika muda tutapitia mafaili kwahiyo wajiandae,” alisema.