Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:39 pm

NEWS: WAANDISHI WA HABARI WAPEWA SOMO.

DODOMA: Waandishi Wa Habari nchini wametakiwa kufanya kazi zao kwa uadilifu ili kuleta uhusiano mzuri kati yako na wabunge.

Hayo yamesema na mhariri mtendaji Wa gazeti La the guardian Jesse kwayu wakati Wa semina ya waandishi Wa habari wanaoripoti habari za Bunge iliyofanyika Leo mjini Dodoma.

Amesema waandishi ni viunganishi kati jamii na viongozi Ili jamii iweze kuwamini ni kufanya kazi bila ubanguzi.

Kwa upande wake mhariri Wa Tanzania Editor forum Neville Meena (TEF) ameongeza kuwa ili kufikisha ujumbe wa ukweli katika mitando ya kijamii ni lazima kupata vielelezo vya kutosha vya habari hiyo kabla ya kuituma.

Amewataka waandishi kuwa waangalifu katika Habari za bunge wanazoandika ili kutoleta sintofahamu kati yao na wabunge.

Nao waandishi wamewaomba wabunge kuepuka kutumia lugha ambazo siyo zuri katika mijadala yao ili kuwaepushia lawama zinazowakabiri za matumizi mabaya ya lugha katika uandishi.

Semina hiyo ya siku mbili ya waandishi wanaoripoti Habari za Bunge hufanyika kila mwaka baadaa ya Bunge kuhairishwa.

Lengo La semina hiyo ni kuwapa mafunzo waandishi kuhusu kuripoti Habari za Bunge.