- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAANDISHI 4 WANUSURIKA KIFO BAADA YA KURIPUKIWA NA GESI
Morogoro. Waandishi wa habari wanne kutoka vyombo vya habari tofauti wamenusurika kifo kwa moto mara baada ya kulipuka kwa mitungi ya gesi kwenye moja ya nyumba mtaa wa Msamvu, manispaa ya Morogoro.
Wanahabari waliojeruhiwa ni Omary Hussein (Star Tv) aliyejeruhiwa mkononi; Hassan Ninga (Imani Media) na Nicholas Mwanaharusi (Global Tv) waliojeruhiwa kila mmoja mguuni na Salum Yusuf (Abood Media) aliyejeruhiwa usoni, mikononi na miguu.
Kwamujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea leo Jumamosi Machi 14, 2020 saa 9:00 alasiri maeneo ya Mafisa katika moja ya nyumba inayohifadhi mitungi ya gesi.
Amesema waandishi hao walifika eneo la tukio kwa nia ya kuchukua habari baada ya kupata taarifa ya kuungua kwa nyumba hiyo.
Amesema mara baada ya kuchukua tukio hilo wakiwa wanaondoka eneo hilo, mitungi mingine ililipuka na kuwaunguza. Amesema hali zao zinaendelea vizuri huku mmiliki wa nyumba na muuza gesi wakitafutwa na polisi.