- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAANDAMANAJI HONG KONG WALIZUIA BUNGE KUJADLI MUSWADA TATA
Polisi wametumia maji ya kuwasha na virungu leo Jumatano kuwapiga na kuwatawanya maelfu ya waandamanaji waliojaribu kuyafikia majengo ya bunge la HongKong.
Hatua hiyo imekuja wakati maandamano dhidi ya muswaada wenye utata kugeuka kuwa vurugu.
Mapambano yalizuka muda mfupi baada ya saa tisa jioni muda wa mwisho uliotolewa na waandamanaji kuitaka serikali kuachana na muswaada huo wa sheria utakaofungua njia ya washtakiwa kupelekwa China kwenda kushtakiwa badala ya nchini kwao.
Waandamanaji wakitumia miamvuli kama ngao walionekana wakijaribu kuwasogelea karibu polisi wa kuzuia fujo wanaolinda jengo la bunge.
Wakiwa wamevalia mavazi meusi na kofia nguvu za kichwa, waandamanaji walikabiliana na polisi waliokuwa nje ya ukumbi wa bunge kujaribu kuwazuia maelfu ya raia wasiingie katika njia za makao makuu ya Serikali.
Mpaka kufikia majira ya asubuhi ya Jumatano, njia zote za kuelekea kwenye ukumbi wa bunge na ofisi za Serikali zilikuwa zimezingirwa na kujaa waandamanaji waliokuwa na mabango wakidai uhuru.
Maandamano ya hivi leo yamechelewesha mjadala wa bungeni ambapo wabuneg walitakiwa kujadili sheria ya kubadilishana wahalifu na Serikali ya Beijing, ambapo unatakiwa kupigiwa kura Juni 20.
Wakiwa wamejihami kwa mabango na vizuizi, waandamanaji walikuwa waakimba nyimbo za kimapunduzi na kuukashifu utawala wa Beijing kwa kujaribu kuingilia masuala yake ya ndani.
Mpaka sasa hakuna taarifa za polisi kutumia mabomu ya kutoa machofu au maji ya pilipili kujaribu kukabiliana na waandanaji ambao wameapa kuhakikisha sheria hiyo haipitishwi.