- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAANDAMANAJI 30 WAUWAWA NCHINI IRAQ
Takribani waandamanaji 30 wameuwawa jana Ijumaa wakati wa wimbi jipya la maandamano ya umma yaliyofanyika dhidi ya serikali nchini Iraq.
Hayo ni kulingana na Mjumbe wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Faisal Abdullah, ambaye amesema vifo hivyo vilitokea wakati polisi ilipofyetua risasi za moto na gesi ya machozi kutawanya waandamanaji.
Watu 8 waliuwawa kwenye mji mkuu Baghdad, wengine 18 katika miji ya Maysan na Dhi Qar, watatu mjini Basra na mtu mmoja aliuwawa kwenye jimbo la kusini la Muthanna.
Kulingana na Abdullah watu wengine zaidi ya 2,300 walijeruhiwa huku takriban majengo 50 ya serikali na ofisi za vyama vya siasa yaliyochomwa moto katika baadhi ya majimbo nchini Iraq.
Marufuku ya kutotoka nje imetangazwa kwenye majimbo ya Dhi Qar, Basra, Muthanna na Wasit.