- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VYOMBO 2 VYA HABARI CONGO WASHIRIKA WA KABILA HATARINI KUFUNGWA
Vituo viwili vya televisheni nchini DRC Congo ambavyo vilikuwa washiriki wa Rais Kabila vya Digital-Congo na Tele 50 vimeshindwa kulipa mishahara wafanyakazi wao kwa miezi kadhaa sasa vinaonekana hatarini kufunga urushwaji wa matangazo kutoka kwenye vyombo hivyo.
Utawala wa zamani na washirika wa karibu wa Joseph Kabila, wameanza kutafuta usuluhu. Vituo hivyo viwili vilianza kukumbwa na hali hiyo baada ya kujiuzulu kwa Moïse Katumbi kama gavana wa mkaa na mkuu wa chama cha PPRD katika mkoa wa Katanga. Alikuwa mojawapo wa wachangiaji wakubwa katika vituo hivi viwili ambavyo vilikuwa karibu na utawala wa zamani wa Joseph Kabila, mbali na kituo cha serikali cha RTNC.
Madai ya wafanyakazi wa Digital Congo na Tele 50 yaliongezeka baada ya mabadiliko katika uongozi wa nchi hiyo. Baada ya kukusanya miezi kadhaa ya madeni ya mishahara, wafanyakazi wa vituo hivi viwili, pia, walianza kujiunga na wenzao katika migomo ya kila mara, kama katika makampuni mengine mengi nchini DRC.
"Tutalipa awamu ya kwanza ya malimbikizo ya mishahara kwa wafanyaazi wa Digital kabla ya siku ya Jumamosi, malipo ya awamu nyingine yatafanyika kabla ya mwezi Juni mwaka huu," amesema Theodore Mugalu. Mkuu wa makaazi ya aliyekuwa rais wa DRC Joseph kabila, ametangaza pia kwamba watapitia upya uongozi wa Digital Congo. Kwa upande wa Tele 50, hali bado ni tete.