- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VYAMA 18 VYAJITOKEZA KUSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa taarifa kwa Umma kuhusu Uchaguzi Mdogowa Udiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 17 Agosti mwaka 2019,kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura Na. 292.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, Utoaji wa Fomu za wagombea ulipangwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Julai hadi 03 Agosti, 2019 na Uteuzi wa wagombea kufanyika jumamosi tarehe 03 Agosti, 2019.
Hadi kufikia jana Agosti 2, 2019 saa 10:00 jioni jumla ya wagombea 60 kutoka vyama vya siasa 18 wamechukua fomu za uteuzi.Vyama vilivyochukua fomu hadi sasa na idadi ya wagombea waliochukua fomu kwenye mabano ni Chama cha DEMOKRASIA MAKINI(5) AAFP (5), CCK(3), DP (4), SAU (4), UDP(4) ACT Wazalendo (3), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), ADA TADEA (4), CHADEMA (2), CHAUMA (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2)na UMD (1).