Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:55 am

NEWS: VIONGOZI WAKUU WA CLUB YA SIMBA WACHIWA KWA DHAMANA

Dar es Salaam. Waliokuwa viongozi wa kuu wa Klabu ya Simba, Sport club ya Jijini Dar es salaam Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyange 'Kaburu' wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea shtaka la utakatishaji wa fedha, huku maombi ya rufaa ya Serikali yakitupiliwa mbali.

Tokeo la picha la aveva na kaburu mahakamani

Septemba 20, mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa kuwafutia mashtaka mawili ya utakatishaji wa fedha Aveva aliyekuwa rais wa simba na makamu wake Nyange, ambapo washtakiwa hao walitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh30 milioni kila mmoja, lakini upande wa Serikali ulikata rufaa kupinga dhamana hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba aliyatupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Serikali ya kupinga uamuzi huo.

"Kitendo cha Serikali kukata rufaa kupitia mawakili wa Serikali haizuii washtakiwa kupewa dhamana, hivyo maombi yaliyotolewa nayatupilia mbali," alisema Baada ya Hakimu Simba kutoa uamuzi huyo,

Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrack Kimaro alidai kuwa hawajaridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo, hivyo wanakwenda kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

"Uamuzi yaliyotolewa sijaridhika nayo, hivyo naenda leo hii kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania," alidai Kimaro. Baada ya Kimaro kueleza hayo Hakimu Simba alisema hata kama wanakata rufaa haitengui uamuzi wa mahakama hiyo na ndipo wakili huyo alipoieleza mahakama kuwa anajiondoa katika kesi hiyo, kisha Wakili Kimaro alinyanyuka na kutoka nje