- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI WAKUU WA CHADEMA WAPEWA SIKU 3 ZA KUJITETEA
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuti Jijini Dar es salaam imewapa siku tatu za kujitetea Viongozi tisa wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe katika kesi ya jinai namba 112 ya 2018.
Mahakama imesema viongozi hao watajitetea kuanzia Novemba 4, 5 na 8, 2019 katika Mahakama hiyo.
Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ametoa uamuzi huo leo Jumatatu Oktoba 21, 2019 mbele ya mawakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya, Hekima Mwasipu na mawakili wa Serikali, Faraja Nchimbi, Wankyo Simon na Salim Msemo.
Hakimu Simba akitoa uamuzi huo amesema wiki tatu zilizoombwa na upande wa utetezi ni nyingi hivyo aliwapatia wiki mbili ili waweze kuwaandaa washtakiwa waanze kujitetea kabla ya mashahidi wao
Hakimu Simba amesema mashahidi katika kesi hii mbali na washtakiwa ni wengi kweli 200 upande wa utetezi wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.
"Kutoka na wingi wa mashahidi hakuna namna kusikiliza kesi hii mfululizo na ni lazima isikilizwe mfululizo itaanza Novemba 4,5 na 8, 2019" alisema Hakimu Simba.
Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya ya Oktoba 18, 2019, Wakili wa utetezi Peter Kibatala kuomba wapatiwe muda wa wiki tatu ili waweze kuandaa washtakiwa na mashahidi wao kwa utetezi.
Awali, Kibatala aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao watatoa ushahidi wao chini ya kiapo kwa kadri dini zao zinavyoruhusu.
Washtakiwa hao wanaanza kutoa utetezi wao baada ya mashahidi nane wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na Mahakama kuwaona washtakiwa hao wana Kesi ya kujibu wajitetee.
Wanaokabiliwa katika kesi hiyo, mbali Mbowe ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar-Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji.
Wengine ni wabunge; John Heche (Tarime Vijijini), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Esther Matiko (Tarime Mjini).
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam