- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI WA HONG KONG WAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO
Muda mfupi kabla ya maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri wa umma wa China, maafisa wa serikali ya HongKong wamepiga marufuku maandamano makubwa yaliyokuwa yafanyike katika jimbo hilo.
Zaidi ya hayo wanaharakati wawili wamekamatwa. Msemaji wa ushirika wa wenye kuandaa maandamano,"Civil Human Rights Front" anasema kamata kamata hiyo imelengwa kuwatisha waandamanaji.
Hata hivyo anasema hawatotishika. Mbali na maandamano hayo yaliyopigwa marufuku, wanaharakati wa vuguvugu la kudai demokrasia wanapanga kuitisha maandamano zaidi kesho Oktober mosi ,siku ya kuadhimisha miaka 70 ya jamhuri ya umma wa China.
Wadadisi wanaashiria wimbi jipya la mapambano kati ya waandamanaji na vikosi vya polisi.