Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:46 am

NEWS: VIONGOZI WA DINI WAONYWA.

DODOMA: VIONGOZI wa dini mbalimbali wametakiwa kuhakikisha wanalinda amani ya nchi na kujiepusha na makundi ambayo yanaweza kusababisha migogoro na kupelekea kuhatarisha amani ya nchi.

Rai hiyo Umetolewa na askofu Mkuu wa kanisa la Baptist,Dorlnad Manase wakati akifungua mkutano mkuu wa 41 wa jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania lililofanyika mjini hapa.

Askofu Manase amesema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kufanya kazi na serikali huku viongozi hao wakikemea vitendo vya wizi,rushwa pamoja na ufisadi.

Katika mkutano huo Askofu Manase alisema kazi kubwa ya kanisa ni kuhakikisha inasimamia taifa katika kutenda haki huku demokrasia inalindwa na kusimamiwa huku katiba ikiwa inalindwa.

“Kanisa haliko tayari kuona nchi inaingia katika machafuko kwa kuwaruhusu watu ambao wanafanya vurugu au kuona katiba ya nchi inavunjwa.

“Lazima tujue kuwa viongozi wote waliopo serikalini wanatokea katika nyumba zetu za ibada,kama kwelitunataka kutunza amani ya nchi ni lazima kukemea na kuonya pale ambapo inaonekana wazi kuwepo kwa uvunjifu wa amani .

“Viongozi wa dini msikubali kujiingiza katika migogoro ya aina mbalimbali iwe makanisani au kujiingiza katika makundi ya kisiasa, badala yake viongozi wa dini wanatakiwa kusimamia haki na kusema ukweli bila kuingiza ushabiki katika mambo ya msingi” alisema.

Katika hatua nyingine askofu Manase amesema kwa sasa kanisa Baptist linafanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya Elimu,afya pamoja na kuisaidia serikali katika kuliombea taifa ili amani iendelee kuwepo.