- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI WA CCM WAPIGWA MSASA JUU YA KATIBA YA CHAMA CHAO
Dodoma: VIONGOZI mbalilmbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kutoa elimu kwa wanachama wao juu ya mabadiliko yaliyofanywa katika katiba ya Chama.
Akizungumza katika semina ya uchaguzi wa ngazi ya Mashina , Kata na Matawi, Katibu wa NEC , Siasa na uhusiano wa kimataifa, Ngemela Lubinga amesema ni lazima mabadiliko hayo yaeleweke vizuri.
Amesema Chama kimefanya mabadiliko hayo ili kiwerze kuewndana na wakati wa sasa kwani mambo mengi yamebadilika.
Katibu huyo alisema ingawa kuna baadhi ya wanachama wataona ni magumu lakini ni lazima kuwepo na mabadiliko kulingana na nyakati za sasa.
“ Ni muhimu kuwepo kwa mabadiliko hayo lakinin pia ni muhimu wanachama wetu wakaelimishwa vizuri juu ya mabadiliko haya’’ alisema.
Alisema nia kubwa ya mabadiliko hayo ni kuleta maendeleo ndani ya Chama na hata nje kwenye jamii.
Akizungumzia chaguzi amesema ni muhimu kwa wanaccm kuwaachia wanachaka kumchagua mtua wanae mpenda badala ya kuwawekea watu.
Katibu alieleza kuwa uchaguzi huo ukifanyika vyema itakuwa rahisi kwa CCM kushinda katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ujao na hata uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Awali akitoa taarifa ya uchaguzi wa CCM wa Wilaya ya Dodoma Mjini Katibu wa CCM Wilaya Pili Agustine alisema uchukuaji wa fomu kwa wanachma imekuwa ukienda polepole.
Amesema hali hiyo inatokana na baadhi ya mashina kutakiwa kuungana ili kufikisha idadi ya wanachama wanaotakiwa kuwa Shina.
Pili alisema ili kuwepo na shina ni lazima kuwepo na wanachama wanaofikia 250.