- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA ARUSHA LEO
Mkutano Mkuu wa viongozi wa mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika leo katika makao makuu ya Jumuiya hiyo mjini Arusha, nchini Tanzania.
Viongozi hao wanakutana baada ya kikao hicho kuahirishwa mara mbili, baada ya Burundi kushindwa kutuma mwakilishi wake.
Uongozi wa Jumuiya hiyo unasema kuwa, ajenda kuu ni kuangazia maendeleo ya mataifa yote sita katika jumuiya hiyo na ripoti zinasema kuwa tofauti kati ya nchi za Rwanda na Burundi, hazitajadiliwa katika kikao cha leo.
Tangu mwezi Oktoba mwaka jana Burundi iliomba tofauti kati ya mataifa hayo mawili ziwekwe kwenye ajenda ya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, bila mafanikio.
Burundi inaichukulia Rwanda kama adui yake mkuu anayelenga kuishambuliwa kwa kuwasaidia wanasiasa wa upinzani na askari wa zamani waliokimbilia nchini humo.
Hata hivyo Rwanda imeendelea kufutilia mbali madai hayo.