- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI CHADEMA KUBURUZWA TENA MAHAKAMANI
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa limekamilisha upelelezi dhidi ya Kesi ya wafuasi 27 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakiwemo viongozi watatu ambao ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya na Meya wa Ubungo Boniface Jacob wanaodaiwa kufanya fujo katika gereza la mahabusu la Segerea
Hatua hiyo imetolewa leo Machi 15, 2020 na Kamanda wa kanda hiyo , Lazaro Mambosasa huku akibainisha kuwa Jalada la Kesi hiyo litatua kesho Jumatatu kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mambosasa amesema kuwa mnamo Machi 13 mwaka huu saa 07:00 mchana jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa gereza hilo kuwa kuna kundi la wafuasi wa Chadema limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo.
Amesema wafuasi hao walifanya vurugu hizo walipokuwa wakienda kumtoa mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambapo walikwenda kufanya vurugu kutaka kumtoa kabla ya kukamilisha taratibu.
“Tulifika eneo la tukio na kukuta askari wa magereza wakiendelea kuwadhibiti wanachama hao ndipo polisi walipowakamata watuhumiwa 27 na kuwapeleka katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano,” amesema.
“Baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeshakamilika,” ameongeza.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa alitumia mkutano huo kutoa rai kwa kikundi chochote cha siasa, dini, au mtu yeyote kuacha kuchezea maeneo nyeti kama vile magereza, makambi ya majeshi yote au maeneo yoyote ambayo ni nyeti kwa kwa Taifa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachokiuka taratibu na sheria zilizowekwa.
“Kwa hiyo niwaombe wananchi wote ndani ya kanda kuheshimu taratibu za nchi na kufuata miongozo yote inayotuweka salama kinyume na hapo mnatuita sisi tufanye kazi yetu magereza ni eneo ambalo linatunza wafungwa ambao wapo kisheria hivyo ni eneo ambalo linapaswa kuheshimiwa,” amesema.
Kwa upanda wao wabunge hao wa Kawe na Bunda leo wameeleza tangu walipofika katika gereza hilo, walivyoshushwa kwenye magari, kupigwa na kisha kupelekwa Kituo cha Polisi Stakishari walikotoa maelezo na kuachiwa kwa dhamana.
Wakati Mdee akisema amevunjwa mkono wake wa kulia, Bulaya alisema ameelezwa kuwa pingili za mgongo zimetikisika kutokana na kukanyagwa huku Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ambaye pia alikuwa na wabunge hao akieleza hali ilivyokuwa.
Mdee, Bulaya na Jacob pamoja na diwani wa Tabata, Patrick Assenga na Katibu wa Chadema Dar es Salaam Kuu, Henry Kileo ni kati ya watu 27waliokamatwa katika gereza hilo walikoenda kumchukua Mbowe.
Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum, Jesca Kishoa na mjumbe wa baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Hadija Mwago.