- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI 8 WA CHADEMA AKIWEMO MBOWE WAKATA RUFAA
Dar es salaam. Viongozi 8 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akiwemo mwenyekiti wao Freeman Mbowe wamekata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 10, 2020.
Viongozi hao 8 na Wanachama wengine wote walitakiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliokuwa yakiwakabili.
Katika kesi hiyo ambayo mshtakiwa wa tisa alikuwa Dk Vicent Mashinji aliyehamia CCM Februari 18, 2020 akitokea Chadema alikokuwa katibu mkuu kuanzia mwaka 2016 hadi Desemba 2019.
Uamuzi wa kuwatia hatiani ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.
Mbali na Mbowe, wengine ni katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika; naibu katibu mkuu-Zanzibar, Salum Mwalimu; Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; Halima Mdee (Kawe); John Heche (Tarime Vijijini); Ester Bulaya (Bunda).
Viongozi wote hao walilipa faini hiyo na kukwepa kifungo chama miezi 5.
Katika rufaa hiyo namba 76 ya mwaka 2020 inayoonyesha kupokelewa Mahakama Kuu Masjala ya Dar es salaam Aprili 8, 2020, inaonyesha warufani nane isipokuwa Dk Mashinji.
Baadhi ya mambo waliyopinga katika hukumu hiyo ni Mahakama ya Kisutu kufanya makosa ya kisheria kufikia maamuzi ya kesi ya msingi bila ya upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo shaka.
Wamedai Mahakama ya Kisutu ilikosea kwa kushindwa kufanya mchanganuo vizuri kwa kufuata ushahidi uliotolewa.
Sababu nyingine waliyoianisha ni mahakama kushindwa kuainisha viini vya makosa dhidi ya mashtaka na kuwahukumu ndivyo sivyo na kutozingatia utetezi wa washtakiwa.
Hoja nyingine ni kupinga hukumu hiyo kutokana na Mahakama kushindwa kuzingatia ushahidi kwa kushindwa kuangalia uwepo au ushiriki wa baadhi ya watuhumiwa kwenye mkutano na kuwahukumu kwenye shtaka la 2,3 na 4.