- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VILIO SIMANZI KUUNGUA KWA SOKO LA MWEMBE TAYARI
Dodoma: Wafanyabiashara wa soko la mwembe tayari,manispaa ya Dodoma wamepata hasara ya mali zao kuteketea kwa moto.
Makamu mwenyekiti wa soko hilo,Aloyce Emanuel Mbolo,amesema zaidi ya vibanda 30 ambavyo vipo ndani ya soko hilo vimeungua.
Amesema majira ya saa nne usiku akiwa nje ya soko hilo akiangalia mpira alishutushwa na moshi mkali ambao ulionekana kuwa mkubwa sokoni hapo huku bila kujua chanzo cha moto.
Hata hivyo amesema chanzo cha moto hakikuweza kujulikana kutokana na soko hilo kutokuwa na umeme jambo ambalo alidai chanzo cha moto uenda ni kutokana na akina mama lishe.
Akizungumzia juhudi za kuzima moto alisema walilazimika kuwaita kikosi cha zima moto licha ya kutumia muda mwingi kufika lakini walifanikiwa kulipa.
Naye mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina moja la Mlaya,alisema yeye ni mfanya biashara wa kuuza spea za magari.
Hata hivyo ameishauri serikali kuwaruhusu wafanyabiashara wa soko hilo kujenga vipanda vya kudumu badala ya kujenga vibanda ambavyo ni hatari zaidi yanapotokea majanga ya moto.