- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIJANA WATAKIWA KUWA MABALOZI WA KULINDA AMANI.
Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,Anthony Mavunde, alipokuwa akifungua kongamano la vijana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kilele cha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mavunde amesema Vijana wanatakiwa kuwa wazalendo katika kuhakikisha wanalinda amani ya nchi na kuepukaba na watu ambao wanalengo la kuwatumia kufanya uchochezi.
Naibu huyo amesema kama taifa halitakuwa na amani ni wazi kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kufanyika.
Mbali na kuwataka vijana kulinda amani Mavunde amewataka vijana kuachana na tabia ya kukaa vijiweni wakipiga soga za kuwasema wanasiasa au kushabikia timu za mpira kwa timu za ndani ya nchi au nje ya nchi.
"Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kukaa vijiweni wakibishania mambo ambayo hayana msingi wa kimaendeleo.
" Utakuta vijana wengi wa kitanzania wanatumia muda mwingi wakijadili timu ya mpira ya Asenol na Manchester au wanabishana kuhusu timu ya mpira ya Simba na Yanga badala ya kutumia muda huo kujadili nini wanaweza kufanya kwa maendeleo yao ya kujikwamua kimaisha"alisema Mavunde.
Katika kongamano hilo mavunde amewataka vijana kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ambayo itawawezesha kujiajiri na kuajiri vijana wengine badala ya kusubiri ajira za serikali.
Mbali na hilo Mavunde amekemea tabia ya vijana ambao wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kusambaza taarifa za uchochezi.
"Kutokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii,serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano TCRA wataendelea kuwafuatilia watu ambao wanasambaza taarifa za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya taifa" alisema Mavunde.
Naye mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN)Fatina Kiluvia,alisema vijana wanatakiwa kuimalisha amani zaidi sambamba na kujikwamua kimaisha.
Mwakilishi huyo amesema ili vijana waweze kujikwamua kimaisha ni lazima wawe wabunifu katika kuibua miradi ya kimaendeleo.
Kilele cha maadhimisho ya vijana kitaifa yatafanyika leo katika viwanja vya mwalimu Nyerere mjini hapa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Jennister Mhagama.