Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:49 pm

NEWS: VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA : ''MUDA WA MKOPO VYUONI UONGEZWE''

DODOMA: Vijana wa mujibu wa sheria Oparesheni Tanzania ya viwanda waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kikosi cha jeshi la kujenga taifa cha 834 makutupora wameziomba taasisi zinazo husika na udahili wa vyuo sambamba na mikopo zifuate silabi ya JKT ili kutoathiri mpango wa Taifa wa mafunzo ya mujibu wa sheria kwa vijana wanaomaliza kidato cha Sita.


Mafunzo wanayopata vijana wa mujibu wa sheria yametajwa kuwajengeauzalendo na ukakamavulakini muda umekuwa mchache kutokana na muingiliano wa udahili wa vyuo hivyo kushindwa kumudu baadhi ya mafunzo.

Mwitikio duniwa vijana wa mujibu wa sheria kujiunga na Jkt imeelezwa ni changamoto huku vijana wengine kushindwa kumaliza mafumafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali.

Jeshi la kujenga Taifa JKT limeiyomba serikali kuendelea kulipatia uwezo jeshi hilo ili liweze kuchukua vijana wengi katika makambi yake.

Akifunga mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana amewataka vijana hao waliohitimu mafunzo yao kutojiingiza katika vitendo viovu.

Jumla ya vijana 964 wamehitimu mafunzo hayo ya awali ya kijeshi kwa mujibu wa sheriatayari kwa maandalizi ya kuendelea na masomo yao yaelimu ya juu