- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIJANA 120 WATUA DOM.
DODOMA: Takribani Vijana 120 ambao ni wahitimu wa shirika la Restless Development wamekutana jijini Dodoma Kwaajili ya kujadili mafaniko ambayo wameyapata kama vijana wa kujitolea .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mratibu wa mradi wa shirika hilo linalohusiana na vijana , Ridhwan Juma, amesema kuwa wanatumia fursa hiyo ya kuwakutanisha vijana kama sehemu ya wao kujuana na kufahamiana.
Aidha, Musa amebainisha changamoto kubwa ambayo imekuwa ikijitokeza wakati wa ufanyaji wa kazi ikiwemo kuwa na muamko mdogo wa vijana .
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari ya Lusta ambayo inapatikana jijini Mwanza Mwalimu Paulo Lurent amesema kazi anayoifanya sasa chimbuko kubwa limetokana na shirika hilo huku akitoa wito kwa vijana kuwa wawe na hali ya kujiam ini katika mambo ambayo wanatakiwa kuyafanya.
Hata hivyo,Taasisi ya Restless Development imekuwa ikifanya kazi ya maendeleo ya vijana kama afya,Ujasiriamali na ushirikishwaji wa vijana katika maendeleo ya kiraia chini ya ufadhili wa ford foundation.