Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:52 pm

NEWS: VENEZUELA YAANZA KUPIGA KURA KUIPA MADARAKA ZAIDI BUNGE

Caracas: Nchi ya Venezuela imepiga kura leo la kulipa bunge Bunge madaraka zaidi nchini humo, Rais Nicolas Maduro wa Venezuela alipiga kura leo Jumapili kuzindua rasmi kura hiyo yenye utata nchini humo kulichagua bunge litakalokuwa na nguvu na kuahidi kwamba litaondoa mzozo wa nchi hiyo kwa kuandika katiba mpya.


Upinzani nchini Venezuela unasema ni juhudi za Maduro ambaye anakumbwa na matatizo kung'ang'ania madarakani kwa kuzunguka nyuma ya bunge ambalo linadhibitiwa na upinzani Televisheni ya taifa imemuonesha maduro akipiga kura katika eneo la magharibi mjini Caracas kwa ajili ya bunge la wananchi litakalokuwa na wajumbe 545 ambalo litakuwa na mamlaka ya kulivunja bunge linalodhibitiwa na wapinzani na kubadilisha sheria wakati likifanya mageuzi ya katiba ya nchi hiyo.