Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:48 am

NEWS: UWT MBARALI INA TEST MITAMBO KATA KWA KATA.

MBARALI: Kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2019 Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imefanya ziara kata kwa kata kuwaandaa wanachama wake na uchaguzi huo.

Akizungumza katika ziara yake Kata ya Lujewa na Isisi Kaimu Katibu wa UWT wilaya ya Mbarali Veronica Mwembezi amesema uchaguzi huo ni muhimu kwa chama kwa kuwa ni mtaji wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.

"Tukiwaelimisha watu wakaona umuhimu wa kushiriki uchaguzi huu 2020 kazi haitakuwa kubwa,lakini pia tukishinda vizuri huu utakuwa ni mtaji wetu mkubwa,"alisema katibu huyo.

Amewataka wanawake wenye sifa kutobaki nyuma bali wajitokeze ili wachaguliwe.

"Wanawake wenzangu msiogope kabisa huu uchaguzi ni wetu sote, ukiona uwezo unao jitokeze usiseme hii nafasi ni ya wanaume hapana, nafasi ni yetu sote alimradi unajua uwezo unao, alisema katibu Veronica.

Ameeleza umuhimu wa kuongeza wanawachama wapya kwa kuwa mtaji wa ushindi unatokana na wanachama.

"UWT imara, tushikamane kuleta ushindi wa tsunami kwa CCM".