Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:45 pm

NEWS: UWAMUZI WA MAHAKAMA KUPINGA MAPENZI JINSIA MOJA WAPOKELEWA TOFAUTI

Mahakama Kuu nchini Kenya jana imetupilia mbali kesi ya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja waliokuwa wanataka kubadilishwa kwa kifungu cha sheria kipengele cha 162 na 165 cha sheria ambavyo vinatoa fursa ya vizuizi vya kisheria kuweza kutumika kwa watu ambao wanahukumiwa na vitendo vya ngono vya watu wa jinsia moja nchini humo.

media

Majaji jijini Nairobi wamesema malalamishi wa wanaharakati hao haikuonesha ni namna gani sheria hiyo iliyotungwa wakati wa ukoloni inavyokwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo na badala yake inatoa nafasi ya usawa kwa watu wote wanaoishi nchini humo.

lakini wakati Uwamuzi huo unafanyika na kutoa ahueni kwa watu waliokuwa wapingaji wakubwa wa vitendo hivyo Vya mapenzi ya jinsia moja Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo ameelezea kusikitishwa na uamuzi wa mahakama kuu ya Kenya ya kukazia hukumu ya sheria ya zama za ukoloni ya kutohalalisha mahusiano ya jinsia moja kati ya watu wazima.

Uamuzi huo wa Majaji hao watatu Roselyn Aburili, Chacha Mwita na John Mativo unamaanisha kuwa mapenzi ya jinsia moja yanasalia haramu nchini Kenya, kwa kile walichosisitiza kuwa sheria hiyo iko wazi na inamlinda kila mmoja.

Watetezi wa haki za binadamu kwa muda mrefu wamesema kwamba mapendekezo haya yanakiuka wajibu wa haki za binadamu wa Kenya na vinachangia katika ukatili na unyanyapaa dhidi ya watu wa makundi ya wasagaji, mashoga, wenye uhusiano wa pande mbili na waliobadili jinsia zao, LGBT.

Bi. Bachelet amenukuliwa katika taarifa akisema, “kufanya kuwa uhalifu vitendo ambavyo vinalenga kundi moja kwa misingi ya wanaowapenda na walivyo ni unyanyapaa. Aidha inatoa ujumbe hatari kwa jamii kwa ujumla na inaibua uhasama n ahata ukatili dhidi ya LGBT.”

Sheria hiyo inaeleza kuwa yeyote atakayeshatakiwa nchini humo kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, atahukumiwa jela miaka 14.

Muungano wa mashoga na wasagaji nchini humo unasema kuwa kumekuwa na kesi 15 dhidi wanachama wao mwaka 2018.

Uaumuzi huo uliotolewa siku ya Ijumaa, uliahirishwa kutoka mwezi Februari.

Kenya ni miongoni mwa mataifa mengi ya Afrika ambayo hayaungi mkono mapenzi ya jinsia moja licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa ya kigeni.