- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UTUNZAJI WA MAZINGIRA BADO KITENDAWILI
DODOMA: IMEELEZWA kuwa kiwango cha hali ya utunzaji wa mazingira nchini hakiridhishi.
Hali hiyo imebainishwa na Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira), kutokana na utafiti uliofanywa na Kituo cha Carbon Monitering umebaini kuwa hali ya utunzaji wa mazingira nchini ni mbaya.
Akizungumza leo mara baada ya kufungua mafunzo ya mazingira yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi Nchini na kuwashirkisha viongozi,wataalam na wadau mbalimbali nchini, Prof Faustin Kamuzora, amesema ramani katika utafiti huo inaonyesha hali utunzaji wa mazingira hasa katika maeneo ya misitu na mimea ni mbaya sana.
Amesema kuwa hali ya utunzaji wa mazingira kufuatana na sayansi inavyoonyesha Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia kituo Carbon Monitoring Center kimetoa ramani ya kuonyesha hali ya uharibifu wa mazingira nchini.
“Ramani hizo zinaonyesha utunzaji wa mazingira hasa misitu na mimea ni mbaya sana,”alisema.
Amesema kuwa hata maeneo ambayo yanajulikana kama hifadhi katikati kunaonekana mimea na miti mingi imeharibiwa.
“Kinachotakiwa kufanywa ni kuelimishana kama hatutahifadhi mazingira hali haitakuwa nzuri na kufuatana na utunzaji wa mazingira unakuta
hata katika mbuga zetu kunaanza kutokea mimea ambayo ni vamizi ambayo si ya asili inaleta shida hata wanyama, ng’ombe hawaili,”alisema.
Hata hivyo, amesema katika eneo la utunzaji wa mazingira kwenye maeneo ambayo ni vyanzo vya maji bado kama nchi haijafanya vizuri na hivyo kuleta matatizo katika uzalishaji wa umeme na matumizi mengine
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja amesema taasisi hiyo ina programu ya kusimamia raslimali za asili na kwamba tatizo lililopo katika usimamizi wa sekta hiyo ni uchafuzi wa
mazingira.
“Sasa lazima wananchi ama nchi itumie raslimali zake lakini izitumie kwa namna ambavyo haichafui mazingira kwasababu itakuwa imeathiri hata vizazi vijavyo,”alisema.
alisema taasisi hiyo ina programu ya kusimamia raslimali za asili na kwamba tatizo lililopo katika usimamizi wa sekta hiyo ni uchafuzi wa
mazingira.
“Sasa lazima wananchi ama nchi itumie raslimali zake lakini izitumie kwa namna ambavyo haichafui mazingira kwasababu itakuwa imeathiri hata vizazi vijavyo,”alisema.