Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:38 pm

NEWS: UTORO KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI UMEISABABISHIA SERIKALI HASARA YA ZAIDI YA SH.BILIONI 700

Dodoma: Tatizo la utoro kwa baadhi wa walimu wa shule za msingi nchini limeisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mia saba kila mwaka kutokana na malipo ya mishahara. .

Ripoti ya utafiti wa Twaweza uliyofanywa kwa muda wa miaka minne imebainisha kuwa tatizo hilo linachangiwa na walimu hao kukosa motisha ya kazi na hivyo kuamua kutoa motisha kwa walimu wa darasa la kwanza hadi la tatu katika wilaya 21 nchini jambo ambalo limetoa matokeo chanya.


Waziri wa nchi anaehusika na tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI George Simbachawene ameitaka taasisi hiyo kuendelea kuibua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu nchini ili serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu waweze kuzifanyia kazi ambapo pia amesema suala la motisha kwa walimu litasaidia kuinua kiwango cha uelewa na ufaulu kwa wanafunzi wengi.


Baada ya miaka miwili ya majaribio, matokeo ya utafili huo yanaojulikana kama Kiu ya Kujifunza yameleta matokeo chanya kwa wanafunzi ambapo walimu zaidi ya mia nane walizawadiwa zaidi ya shilingi milioni mia mbili.

Hivi karibuni Taasisi ya Twaweza ilitoa tathmini ya ripoti ya mwaka 2011 na 2015 ambayo ilionyesha nusu ya wanafunzi wa darasa la saba nchini hawawezi kufanya majaribio ya darasa la pili kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro wa walimu, wanafunzi pamoja na matabaka katika familia.