- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ''UTOAJI WA TAKWIMU BILA USHAHIDI WA KISAYANSI NI KOSA'', DK KAPOLOGWE.
DODOMA: Mkurugenzi wa huduma za afya Ustawi wa jamii na lishe Dk. Ntuli Kapologwe kutoka ofisi ya Rais (TAMISEMI) amesema utoaji wa Takwimu bila ushahidi wa Kisayansi ni kosa na inaweza kupelekea kufanya maamuzi ambayo siyo sahihi.
Pia amewataka waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuanzia mwaka huu kutenga fedha kwa ajili ya ushiriki wa makongamano ya afya hususani ya ufuatiliaji takwimu ambazo zitawasaidia kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya.
Dk. Kapologwe ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa kongamano la tatu la afya lililoandaliwa na Chuo kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na St Francisco ambalo lilijumuisha wataalamu wa sekta hiyo toka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Kutokana na hilo amesema waganga wa mikoa na wilaya kuanzia mwaka huu wanapaswa kutenga bajeti ya fedha ambayo itawasaidia kushiriki katika makongamano kama haya ili iwe rahisi kuwa na takwimu sahihi pale wanapoulizwa kuhusu jambo flani.
"Serikali tunachkulia umuhimu kongamano kama hili kwa sababu takwimu ni muhimu kwa kila sekta sio Wakuu pekee," alisema Dk Kapologwe.Mbali na hilo alisema TAMISEMI inahusika na ujenzi wa vituo vya afya na hospitali hivyo kipitia kongamano hili tunakaribisha vyuo kuja kufanya utafiti ili kutoa takwimu sahihi kuhusiana na ujenzi huo kama msongamano wa wagonjwa umepungua.
"Tunawakaribisha mje mfanye tafiti katika vituo vya afya vilivyojengwa ili kuona huduma ikoje na upungufu wa vifo vya kinamama na watoto ", amesema Dk Kapologwe.
Amesema mkifanya hivyo itasaidia kujua takwimu sahihi kulingana na kilichokiwa awali na hivi sasa kupitia takwimu ambazo zimetolewa na watafiti.Alisema tafiti hizo ziunganisje suala la.Sera na utekelezaji kutokana na kwa hiyo ndio dunia ya kisasa ambayo inapiga hatua katika Maendeleo,hasa ukizingatia tunaelekea katika uchumi wa kati wa viwanda ifikapo 2025.
Amesema na utafiti ambao mnafanya uwe we uhakika na ambao utawasaifia wahusika kufanya marekebisho wapi walipokosea.Naye Naibu Makamu mkuu wa chuo Profesa Ganka Nyamsogoro alisema anaiomba serikali iweke mikakati wa kufuatilia makongamano yanayofanyika ili yaweze kuketa matokeo chanya kwa jamii hasara ukizingatia yanafanyika mwaka hadi mwaka.
Amesema ujio wa Mgeni rasmi ni dhahiri serikali iko pamoja na waandaaji wa kongamano hilo ambapo alisema Mrafi huu unaelekea kuisha hivyo ni vema kuona.namba.gani ya kufanya katika hilo.Alisema lengo ni kuona Mradi huo unaelendelea ili kusaidia kutoa uwelewa kwa jamii inayotuzunguka.