- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UTETEZI WA MBOWE WAITAKA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI HOJA ZA SEREKALI
Dar es salaam Wakili Upande wa Utetezi unaomtetea Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe na Esther Matico Piter Kibatala amedai sababu za rufaa za DPP zilizotolewa leo Feb 18 hazina mashiko hivyo ameiomba Mahakama ya Rufani kuitupilia mbali rufaa hiyo
Ombi hilo la Kibatala limekuja mara baada ya Upande wa Mashtaka kuwasilisha hoja mbili za rufaa katika Mahakama ya Rufani huku wakiomba rufaa namba 344 iliyopo Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika itupiliwe mbali kwa sababu haiendani na kifungu cha 362 (1) cha sheria ya Makosa ya Jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo.
Kwa mujibu wa sheria hiyo rufaa ni lazima iambatanishwe na mwenendo wa kesi na uamuzi mdogo unaobishaniwa katika Mahakama Kuu lakini upande wa utetezi hawakufanya hivyo. Rufaa hiyo ilikatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mhazini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.
DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana.
Wakili Mkuu wa Serikali Faraja Nchimbi amedai leo Jumatatu Februari 18, 2019 mbele ya jopo la majaji watatu Stella Mgasha, Gerald Ndika, Mwanaisha Kwaliko wa Mahakama ya Rufani kuwa wanapinga uamuzi uliotolewa na Jaji Rumanyika katika rufaa namba 344 ya 2018 uliotolewa Novemba 30, 2018.
Akitoa hoja ya kwanza ya Rufani yao wakili Nchimbi amedai Jaji Rumanyika alipotoka kisheria kwa kuipanga na kuiita kwa ajili ya usikilizwaji huku akijua rufaa hiyo iliwasilishwa kinyume na kifungu cha 362 (1) cha sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo 2002
Pia wanadai Jaji Rumanyika alijipotosha kwa kushindwa kuwapatia haki ya kutosha ya kusikilizwa.
Kwa upande wa Wakili Peter Kibatala alidai kuhusu lalamiko la kuwa hawakupewa muda wa kutosha wa kusikilizwa, rufaa iliyopo Mahakama Kuu haikusikilizwa na kwamba kilichosikilizwa ni mapingamizi pekee tu.
Hata hivyo, Jaji Mgasha kwa niaba ya jopo amesema watazingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili na kwamba watatoa uamuzi katika tarehe itakayopangwa.