- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UTAJIRI WA MO WAPOROKO KWA BILIONI 700
Dar es Salaam. Mfanyabiasha wa Kitanzania na Mmiliki wa Kampuni ya Mohamed Enterprise Tanzania LTD (MeLT) Mohammed Dewji maarufu kama Mo ametajwa kuwa kwenye nafasi ya 16 kwenye orodha ya Mabilionea 20 Barani Afrika kwa mwaka 2020 licha ya utajiri wake kuporomoka kwa Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni)
Tafiti hizo zimetolewa jana na Jarida mashuhuri la Forbes kwa mwaka huu limemtaja Mo mwenye miaka 44 kama bilionea namba 16 akiwa ndio mtanzania pekee kwenye Orotha hiyo na Bosi wa Afrika Aliko Dangote wa Nigeria akiongoza orodha hiyo na Utajiri wake ukiwa Umepungua kwa Dolla milioni 200.
Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.6 (Sh3.69 trilioni) na anayeshikilia namba moja utajiri wake ni Dola bilioni 10.1 (Sh23.31trilioni) naye utajiri wake ukiwa umepungua kutoka bilioni 10.3 (Sh23.78 trilioni) mwaka jana.
Katika orodha ya jarida hilo mwaka jana Mo ambaye ni raia wa Tanzania anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 14 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.9 (Sh4.3trilioni) hivyo kwa mwaka huu ameshuka nafasi tatu.
“Imepungua Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni), lakini nina watu 32,000 na mwaka huu natarajia kuwekeza Sh500 bilioni hapa hapa nchini na uwekezaji huo utatoa ajira 100,000 kwa Watanzania,” alisema Mo baada ya ripoti hiyo akiwa ndiye Mtanzania pekee aliyeingia katika orodha hiyo.