- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: USHAHIDI WA CD WAKWAMISHA KESI YA ZITTO KABWE
Mahakama ya Hikimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imeahirisha Kesi ya Uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe hadi Desemba 4, 2019.
Hatua ya kuhairishwa kwa kesi hiyo inakuja mara baada ya kuwepo kwa mvutano wa mawakili kutoka pande mbili juu ya Hakimu kupokea/kutokupokea ushahidi wa "CD"
Tayari zaidi ya mashahidi 12 wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, John Makungu.
Katika kesi ya msingi, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho.