- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: URUSI YAONGOZA KUWA NA VICHWA VINGI VYA NYUKLIA DUNIANI
Kwa mujibu wa shirika linalochunguza biashara ya silaha Duniani, SIPRI. lenye makao yake makuu nchini Sweden, limesema kuwa nchi ya Urusi ndio nchi inaongza kuwa na vichwa vingi vya Nyuklia katika nchi 9 duniani zenye silaha hizo.
Nchi zenyewe zenye ni Urusi, Marekani, China, Uingereza, Ufaransa, India, Pakistan, Israel na Korea Kaskazini.
Urusi inavyo vichwa vya nyuklia 6,500 na inafuatiwa na Marekani yenye vichwa vya 6,185 vya silaha hizo. Robo ya silaha hizo ziko katika utayarifu wa mashambulizi wakati wowote.
Katika nafasi ya tatu inakuja Ufaransa iliyo na vichwa vya namna hiyo 300, ikifuatiwa kwa karibu na China ambayo inavyo 290. Uingereza inavyo 200, Pakistan 160, India 140, nayo Israel inavyo vichwa vya nyuklia vipatavyo 90.
Ripoti ya SIPRI inasema kwa pamoja nchi hizo zina vichwa vya nyuklia 13,865 mwaka huu wa 2019, vikijumuishwa vile ambavyo havijaunganishwa kwenye makombora, na vilivyo kwenye orodha ya kukongolewa.
Idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ya mwaka 2018, ambapo nchi hizo zilikuwa na jumla ya vichwa 13,925.
Hiyo inamaanisha kuwa vichwa 600 vya nyuklia vilikongolewa, mchakato huo ukiongozwa na Urusi na Marekani chini ya makubaliano yajulikanayo kama START mpya.
Lakini mchakato huo wa kupunguza zana za kinyuklia hautarajiwi kuendelea baada ya mwaka 2021 ambao ni mwisho wa mkataba wa START mpya baina ya Urusi na Marekani, kwa sababu hakuna mazungumzo yoyote yanayofanyika kwa nia ya kuurefusha