Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:49 am

NEWS: URUSI YAGOMA KUIWEKEA VIKWAZO KOREA KASKAZINI

Moscow: Waziri wa mambo ya njee wa Urusi Sergei Lavrov ameionya Marekani kupendekeza mazungumzo zaidi kuliko kuiweka vikwazo zaidi Korea Kaskazini

Lavrov amemueleza Waziri wa Ulinzi wa Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini ni kama kumwagia maji kwenye mgongo wa bata.

Hata hivyo Bw.Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.

Waziri wa Ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini.

Kulingana na taarifa ya wizara ya kigeni ya Urusi, Sergei Lavrov na Rex Tillerson walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Korea Kaskazini.

Siku moja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani jaribio la Korea Kaskazini Siku ya Jumatano, rais wa Marekani Donald Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo na Korea Kaskazini sio suluhisho.

Mapema wiki hii Korea Kaskazini ilirusha kombora lake la masafa marefu lililopitia juu ya anga ya Japan, kitendo ambacho Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alisema ni uchokozi wa Korea Kaskazini unaoendelea.