- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: URUSI NA MAREKANI ZARUSHIANA MANENO MKUTANO WA UN
NEW YORK:Majibizano makli yametokea kati ya Balozi wa Marekani Umoja wa mataifa (UN) Nikki Haley na Balozi wa Urusi Umoja wa mataifa Petr Iliichev ambapo Haley ameituhumu Urusi kwa kuulinda uatawala wa Syria katika matumizi yake ya silaha za kemikali na kuzuwia misaada kuwafikia mamia kwa maelfu ya watu waliozingirwa.
Majibizano hayo makali yalitokea wakati wa mkutano wa kila mwezi wa baraza la usalama kuhusu hali ya kibindamu nchini Syria. Awali balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Petr Iliichev alisema kwamba kwa ujumla, mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa Desemba 30 unaendelea kuheshimiwa, ingawa kulikuwepo na mienendo ya yale alioyaita makundi ya kigaidi, na matukio yanayoudhoofisha mpango huo, ambayo yanaathiri ufikishaji wa misaada.
Mkuu wa misaada ya kibidamu wa Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien aliliambia baraza kuwa hali mbaya ya kibinadamu inazidi kudorora, na kufahamisha kuwa hakuna hata msafara mmoja wa misaada umeweza kufika katika maeneo yaliozingirwa nchini Syria mwezi huu, kutokana na kukosa ruksa, hasa kutoka serikali ya rais Bashar al-Assad.
"Wakati ukosefu wa usalama unasababisha hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi kwa mamia ya maelf, njia za kuwapatia msaada unaoweza kuokoa maisha zinazuwiwa kila mara. Natiwa wasiwasi na kuongezeka, narudia -- kuongezeka, katika vikwazo vya kiutawala na ukiritimba mwingine kwa pande zote," alisema O'Brien.
Haley alivituhumu vikosi vya serikali ya Syria kwa kuchukulia ugavi wa dawa - kikiwemo chakula cha watoto, mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo kutoka kwenye misafara ya misaada na kuviuza kwenye soko la magendo kwa bei za juu, baadhi vikiuzwa katika maeneo yanayokumbw ana mashambulizi ya mara kwa mara, na kusema hii ni biashara kubwa nchini Syria.
"Wengi wenu mmesema tunahitaji kuuwekea shinikizoutawala wa Syria. Hivyo sivyo ilivyo. Tunahitaji kuiwekea shinikizo Urusi, kwa sababu Urusi inaendelea kuulinda utawala wa Syria. Urusi inaendelea kuwaruhusu kuzuwia misaada ya kibinadamu kuwafikia watu wanaoihitaji," alisema Balozi Haley.