Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:53 am

NEWS: URUSI INAJIANDAA KUZIMA INTENETI KUJILINDA NA MAADUI ZAKE

Taifa la Urusi linajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda flani, lengo likiwa ni kujitoa kwenye ramani ya mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao na kivita yanayofanyika kwasasa Duniani.(Reuters wanaripoti)

Wachambuzi wa maswala ya kiusalama wanasema lengo muhimu kabisa katika zoezi hilo la Urusi ni kwamba nchini hiyo inajiandaa kuishi bila kuitegemea Dunia hata kama ikitokea nchi zingine zitaitenga nchini HIYO.

Baada ya zoezi hilo litapelekea mawasiliano baina ya raia wa Urusi na mashirika yake kubaki ndani ya nchi badala ya ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.

Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe mosi Aprili, lakini siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.

Nchi wanachama wa Nato na washirika wake wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.

Njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.

Mwishowe, serikali ya Urusi itakuwa na ubavu kama wa China wa kupanga mawasiliano gani raia wake wapate kutoka nje ya nchi.

Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa watoa huduma za intaneti nchini humo wanakubaliana na mabadiliko hayo lakini wanatofautiana kwenye namna gani utekelzwaji wake uwe. Wanaamini jaribio hilo litazaa "mvurugano mkubwa" kwa matumizi ya mtandao ya nchi hiyo, umeandika mtandao wa ZDNet.