Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:55 pm

NEWS: UPINZANI RWANDA WAPINGA URUSI KUJENGA NISHATI YA NYUKLIA RWANDA

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Green nchini Rwanda, Frank Habineza amepinga mpango wa nchi yake kujenga kiwanda cha nyuklia kwa ushirikiano na Urusi akisema utakuwa na athari mbaya kwa wananchi.

Kinu cha Arak chenye madini ya plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.

Akizungumza na kituoa cha habari cha BBC Habineza amesema wao hawakuunga mkono ushirikiano huo baina ya serikali ya Rwanda na Urusi kutokana na athari zake.

"Kulikuwa na mapatano ya Vienna kuhusu maswala ya nyuklia, na wakati huo huo Rwanda ilisaini mapatano mengine na Urusi kuanzisha kiwanda cha nyuklia hapa Rwanda. Mapatano ya Vienna yalikuwa kama kupalilia njia ya hayo ya Urusi kuanza kutekelezwa."

Frank Habineza

"Bungeni sisi hatukupigia kura mswada huo kwa sababu tuliona kwamba bado ni mapema kwa nchi ya Rwanda kujiingiza katika kuidhinisha matumizi ya nishati ya nyuklia kwa sababu sehemu zote kulikojengwa nyuklia kumekuwa na athari mbaya kwa wananchi na kwa mataifa yenyewe" amefafanua.

Kiongozi huyo wa upinzani ametaja mfano wa nchi ya Ukraine ambako kiwanda cha nyuklia kililipuka na kuathiri nchi jirani ya Sweden.

Frank Habineza ni mbunge katika bunge la taifa, na chama chake cha Green kina uwakilishi wa viti viwili tu bungeni.

Muswada huo wa ujenzi wa nguvu za nyuklia ulipitishwa bungeni Rwanda isipokuwa pingamizi ya wabunge wawili tu ambao hawakuunga mkono.