Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:12 am

NEWS: UPINZANI NCHINI KENYA WAPANGA KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA LEO

Nairobi: Muungano wa upinzani nchini kenya NASA unao ongoza na Raila Odinga umesema utafanya maandamano makubwa leo siku ya Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.

Raila Odinga akiwa na muungano wa NASA


Muungano wa NASA umekanusha taarifa zilizotolewa hapo awali, kuwa katika maandamano hayo upinzani utovamia makao ya tume ya ya uchaguzi IEBC kuwatimua kwa nguvu maafisa wa tume hiyo. Hata hivyo NASA imebaini kwamba maandamano hayo yatakuwa ya amani.

“Maandamano haya yana lengo la kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume ya uchaguzi (IEBC) walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi ambao ulifutwa na Mahakama Kuu nchini, ” NASA imesema kataika taarifa yake.

Maafisa wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC)


NASA inataka jumla ya maafisa 12 wa tume hiyo washtakiwe kwa kutowajibika katika uchaguzi uliofutwa wa Agosti 8. Unataka pia mfumo wa teknolojia uliotumiwa wakati wa uchaguzi huo ubadilishwe.

Naye kwa Upande wa Rais Uhuru Kenyatta ameonya waandamanaji kuwa watakabiliwa na hatua kali za sheria iwapo maandamano yao yatasababisha shughuli za kiuchumi za raia zinakwama.

Rais Uhuru Kenyatta