Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:52 am

NEWS: UPINZANI NCHINI ANGOLA WAPINGA MATOKEO YA AWALI

Dar es salaam: Chama kikuu cha Upinzni nchini Angola (UNITA) kimepinga matokeo baada ya kutangazwa kwa matokeo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo, wakala wa chama cha Unita alisimama kupinga matokeo yote kwa jumla mbele ya waandishi wa habari. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, chama cha Unita kilichukua nafasi ya pili na kimepata 24.04% ya kura. Kwa upande wa chama cha upinzani cha kihistoria kimesema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeegemea kwa chama tawala cha MPLA.

Chama hiki kimeahidi kura zake lakini tayari kimetangaza kuwa kimeshinda katika jimbo la Luanda, tofauti na matokeoyaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE) ambayo imekipa ushindi chama cha MPLA.

Kulingana na matokeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, chama tawala kimeshinda katika mikoa yote, ingawa kura zake ziko chini ya zile kilizopata mwaka 2012 katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na zile kilizopata katika mji mkuu Luanda.

Chama cha MPLA madarakani kwa miongo minne nchini Angola kimeshinda Uchaguzi Mkuu kwa 64.57% ya kura, kwa mujibu wa takwimu za awali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kikiongoza mbele chama cha Unita ambacho kimepata 24.04%, Casa-Ce (8.56%) , PRS (1.37%), FNLA (0.95%) na APN (0.52%).