- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UPINZANI BUNGENI WATAKA KUPEWA NAFASI ZA KUCHANGIA
Dodoma. Mnadhimu mkuu wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni, Ester Bulaya ameliomba Bunge la Tanzania kuongeza idadi ya wabunge hasa wa Upinzani kuchangia taarifa za kamati za chombo hicho cha Dola zilizowasilishwa bungeni leo Jumanne Februari 4, 2020.
Leo wabunge wanajadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati tatu za utawala na Serikali za mitaa, katiba na sheria pamoja na sheria ndogo.
Akiomba mwongozo wa Spika bungeni leo Mbunge huyo Bunda Mjini, amesema hawawezi kuwanyima wabunge hasa wa upinzani kutoa maoni yao kwa kamati muhimu kwa sababu ya kisingizio cha muda.
“Kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge kiti chako kinaweza kuongeza muda hadi pale shughuli zitakapokamilika. Mwenyekiti hatuwezi kuwanyima wabunge hasa Kambi Rasmi ya Bungeni kutoa maoni yao katika kamati muhimu za leo,” amesema.
Amesema wanaomba wapewe nafasi za nyongeza za kuchangia ili wabunge wapate nafasi za kutoa maoni yao. “Tunajadili kamati mbili upande wa Chadema tunapata, CUF wanapata nafasi ya ziada, leo tunajadili kamati tatu mnatoa CUF nafasi moja na Chadema nafasi mbili,” amesema. Ameomba haki itendeke kwa vyama hivyo katika nafasi za uchangiaji.
Akijibu suala hilo mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesema ratiba za Bunge zinaenda kwa mujibu wa utaratibu na kwamba ratiba yao ya leo nafasi za Chadema ni mbili na CUF ni moja. “Kwa hiyo kama mnataka kuchangia zaidi mgawane dakika kazi itakwenda,” amesema Najma na kuruhusu kuendelea na shughuli zilizopangwa.